Michezo

“Pogba amekosa furaha ndani ya United” kocha wa Ufaransa ‘Deschamps’

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema kuwa, Paul Pogba katika kipindi hiki amekosa furaha ndani ya Manchester United.

Pogba mwenye umri wa miaka 25 amerejea Old Trafford akitokea Juventus kwa dau la pauni milioni 89 mwezi Agosti mwaka 2016 chini ya kocha,  Jose Mourinho na tayari ameshaonekana kutolewa ndani ya kikosi cha ‘first eleven’ katika michezo mitatu iliyopita.

Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji 25 ndani ya kikosi cha kocha Mfaransa kitakacho shuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki mwezi huu dhidi ya Colombia na Urusi.

Sifahamu hasa juu ya swala hili, ila nina hakika nitasikia juu ya hili bila shaka, ni hali ambayo hafurahi.

Hivi ndivyo mambo yanavyokwenda pengine zipo sababu, nina mambo mengi ya kuzungumza na wachezaji kambini na kufahamu hisia zao na siyo Paul peke yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents