Michezo

Pogba apigilia kinyago cha bei mbaya kabla ya FA Cup (+Picha)

Ukiwa unaweza kuingiza mshahara wa paundi 165,000 kwa wiki unakila sababu ya kufurahia maisha kwa kuwa na vitu vinavyoendana na thamani ya hadhi yako.

Paul Pogba akiwa amevalia kinyago cha OPERA LED chenye thamani ya paundi 1,987 

Na hiyo ndiyo inayotokea kwa staa wa Manchester United, Paul Pogba ambae anakabiliwa na mchezo wa FA Cup dhidi ya Derby.

Pogba akiwa anavishwa kinyago katika hatua za awali

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hapo jana siku ya Jumatano  kiungo huyo wa Ufaransa ametupia picha akionekana amevaa kinyago usoni  ambacho kinagharama ya paundi 2,000.

Kinyago hicho kinachofahamika kama OPERA LED kinachoziba maeneo ya usoni mpaka kwenye shingo na kisicho maumivu husaidia kulaini ngozi na kuifanya kuwa salama.

Tovuti rasmi ya The OPERA imeeleza kuwa kinyago hicho kimekuwa kikivaliwa na baadhi ya watu maarufu na wenye majina makubwa kama, Jessica Alba, Kate Hudson na Chrissy Tiegen,hii ikiwa ni pamoja na mke wa Steven Gerrard, Alex.

Pogba ameyafanya hayo katika kipindi hiki ambacho United inakabiliwa na mchezo wa FA Cup siku ya Ijumaa dhidi ya Derby County.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents