Michezo

Pogba auponda mfumo wa Mourinho wa kulinda zaidi badala ya kushambulia

Pogba auponda mfumo wa Mourinho wa kulinda zaidi badala ya kushambulia

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na kile kinachomsumbua kwenye akili yake baada ya timu yao kupata sare na Wolves nyumbani Old Trafford. Kiungo huyo Mfaransa amefunguka na kuudhihaki mfumo wa kocha wake Jose Mourinho wa kulinda zaidi badala ya kushambulia kitu ambacho kitapelekea kuweza kushinda katika michezo yao.

Licha ya kuuponda mfumo wa kocha wake lakini Pogba amewashauri wachezaji wenzake kuwa wakiwa katika uwanja wa nyumbani Old Trafford wanahitaji kushambulia zaidi badala ya kucheza mfumo wa kulinda zaidi,akiutolea mfano mchezo wao dhidi ya Wolves siku ya jumamosi baada ya timu hiyo kulazimishwa sare na vijana hao wa Moutinho.

” Tukiwa nyumbani tunatakiwa kushambulia,kushambulia,kushambulia zaidi na hivyo ndio inavyotakiwa ukiwa nyumbani” aliongeza Pogba

” Ukiwa nyumbani unatakiwa kucheza vizuri zaidi ya mgeni tena na Wolves tulitakiwa kucheza vizuri zaidi yao,tulitakiwa kushabulia zaidi ili tupate ushindi,timu huwa zinaogopa zinapoiona Manchester inashambulia zaidi na hapo ndio udhaifu wetu”

” Nahisi mtazamo wetu unapaswa kubadilika na kuwa bora zaidi na tunapaswa kucheza vizuri hasa tukiwa Old Trafford na tunapaswakuongeza mashambulizi zaidi kama tulivyofanya na Tottenham, Liverpool, Chelsea na Arsenal msimu uliopita tukicheza hivyo itakuwa rahisi kwetu”

Manchester United wako nafasi ya 7 wakiwa na alama 10huku wakicheza michezo 6 wakishinda 3 wakipoteza michezo 2 na kupata sare mchezo 1.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents