Michezo

Pogba awanunulia wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa pete za thamani kubwa, kama ukumbusho baada ya kutwa kombe la dunia (+ Video)

Mchezaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Labille Pogba ameamua kuwanunuliwa wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ufarnsa Pete ikiwa kama ishara ya ukumbusho baada ya kutwaa taji la kombe la dunia.

Pogba na wengine walizifunua pete, ambazo zimefanyika zikilingana na zile zinazotumiwa na timu za michuano ya NBA na NFL, kwenye vyombo vya habari vya Jumatano.Pogba alisema Antonine Griezmann pia alisaidia katika kubuni pete hizo, ambayo ina alama ya timu ya taifa ya Ufaransa na yenye maneno “Mabingwa wa Dunia.”

Pete hizo pia zina pande tatu zinazovutia za almasi nyeupe, rubi na samafi, kulingana na TMZ.

Pete hizo zinajumuisha kila jina la wachezaji wote walioshiriki katika michuano ya kombe la dunia na upande mwingine zikiwa na jina la ‘mabingwa wa Kombe la Dunia’ kwa upande mwingine, na orodha ya matokeo katika Urusi ya mwisho ya majira ya joto.

Akiongea na waandishi wa habari Pogba alisema:- “Ni zawadi ndogo baada ya kushinda Kombe la Dunia na wachezaji wenzangu,” Pogba alisema katika mkutano wa waandishi wa habari katika kituo cha mafunzo nchini Ufaransa. “Ninawahesabu kuwa familia yangu. Ni zawadi ndogo kutoka kwangu.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents