Michezo

Pogba hana mpango na unahodha United ataka kutimkia Hispania

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba anahitaji kuondoka ndani ya klabu hiyo na kuhamia kwa miamba ya soka ya Hispania Barcelona licha ya tofauti zake na Jose Mourinho kumalizika.

10th August 2018 – Premier League – Manchester United v Leicester City – Paul Pogba of Man Utd – Photo: Simon Stacpoole / Offside.

United imeendelea kusisitiza kuwa kiungo wake aliyesajiliwa kwa rekodi ya dunia pauni milioni 89 haitamuuza licha ya Pogba kuonesha dhamira yake ya kutimkia Hispania.

Meneja wa United, Mourinho anajaribu kumtuliza kiuongo huyo raia wa Ufaransa kwa kumpatia kitambaa cha unahodha ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lakini baada ya mchezo wao wa kwanza wa ligi, Pogba amesema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyo fanyika mpaka kilakitu kitakapo anza kuwa sawa.

Hataivyo wakala wa Pogba, Mino Raiola anachaguo la kumuuza Barcelona au Real Madrid jambo United huenda ikaweka rekodi ya dunia katika mauzo yake.

Pogba mwenye umri wa miaka  25 alianzia kwenye mikono ya meneja Sir Alex Ferguson ndani ya United kisha kuuzwa katika klabu ya Juve mwaka 2012.

Related Articles

6 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents