Michezo

Poland yatinga kombe la dunia 2018, Lewandowski aweka rekodi

Timu ya taifa ya Poland imefanikiwa kukata tiketi ya kufuzu kushiriki michuano ya kombe la duniani nchini Urusi mwakani baada ya kuifunga Montenegro kwa jumla ya mabao 4-2 mchezo uliyopigwa jana siku ya Jumapili.

Kikosi cha timu ya taifa ya Poland

Katika mchezo huo straika wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski ameweka rekodi ya kufunga jumla ya mabao 16 katika michuano hiyo ya kombe la dunia.

Straika wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski

Baada ya ushindi huo straika wa Poland, Robert Lewandowski amesema “Nilikuwa na hasira tulikuwa tukiongoza kwa mabao 2- 0 tena nyumbani lakini ghafla ya karudi. Tukaamua kuongeza latatu na la nne,” amesema Lewandowski ambaye ameweka rekodi ya kufunga mabao 16 na kumzidi Cristiano Ronaldo mwenye mabao 15.

Mabao ya Poland yamefungwa na Krzysztof Maczynski , Kamil Grosicki na Robert Lewandowski kwa upande wa Poland wakati timu ya taifa ya Montenegro ikipata mabao yake kupitia kwa wachezaji  Stefan Mugosa na Zarko Tomasevic.

Katika mchezo huo wa kundi C, Meneja wa timu ya taifa ya Poland, Adam Nawalka amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kuhakikisha wanatoka na ushindi katika mchezo huo muhimu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents