Habari

Polisi akutwa uchi akimbaka mahabusu kituoni

Koplo wa polisi, Onesphory Materu (40) aliyekuwa zamu kituoni, alifumwa uchi wa mnyama akimbaka mahabusu ambaye ni msichana mwenye umri wa miaka 15, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Bw. Issaya Mngulu, amesema.

Na Lulu George, PST Tanga

Koplo wa polisi, Onesphory Materu (40) aliyekuwa zamu kituoni, alifumwa uchi wa mnyama akimbaka mahabusu ambaye ni msichana mwenye umri wa miaka 15, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Bw. Issaya Mngulu, amesema.

Kamanda Mngulu, amesema kutokana na hali hiyo, askari huyo ametimuliwa kazi na sasa atashitakiwa katika mahakama ya uraiani kwa kosa la kubaka .

Msichana huyo (jina limehifadhiwa), aliyekuwa mfanyakazi wa ndani, aliwekwa mahabusu katika kituo hicho cha polisi kwa tuhuma za kumuibia mwajiri wake fedha taslim na vitu mbalimbali.

Kamanda Mngulu, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25, mwaka huu na kwamba kufukuzwa kazi kwa askari huyo, kumefuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kijeshi.

Alisema askari huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho akiwa zamu katika chumba cha mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Lushoto, mkoani Tanga.

`Koplo huyo akiwa zamu, mchana wa siku hiyo ya Jumamosi, alimwendea binti huyo aliyekuwa mahabusu katika kituo hicho na kumtaka kimapenzi,` alisema Kamanda Mngulu.

Aliongeza kuwa, wakati akimweleza hayo, askari huyo alimuahidi msichana huyo kuwa atamuachia huru iwapo atamkubalia ombi hilo.

`Lakini binti naye alikuwa mjanja, kwani alimwambia ahadi hiyo aiweke kwa maandishi ili kuthibitisha maneno yake ya kumwachia huru na ndipo Koplo Materu alipomwandikia na kugonga muhuri wa polisi, kisha akasaini sahihi yake,` alisema Kamanda Mngulu.

Alisema baada ya binti yule kupewa karatasi hiyo, aliiweka mfukoni na kuvua nguo zake na Koplo huyo aliendelea kufanya naye mapenzi.

Alisema wakati akiendelea kufanya hivyo, watuhumiwa wengine wanaume waliokuwa chumba kingine cha mahabusu, waliomba msaada wa kupelekewa ndoo ya kujisaidia, lakini askari huyo alikuwa bize akifanya mapenzi na mtuhumiwa huyo.

Alisema baada ya Koplo huyo kumaliza kufanya mapenzi na binti huyo, na kabla hajavaa nguo zake, askari wengine waliokuwa wakiingia kituoni kumpokea zamu, walimkuta mwenzao akiwa uchi wa mnyama.

Kamanda Mngulu, alisema Koplo huyo aligundulika kwamba kuwa kwake uchi kunatokana na kufanya kitendo hicho baada ya binti huyo kuonyesha

Alisema binti huyo anayefanya kazi ya ndani, mkazi wa Masiwani jijini Tanga, alifikishwa kituoni hapo kwa tuhuma za kumwibia mwajiri wake Sh. 70,000 na vitu vingine mbalimbali, vyote vikiwa na thamani ya Sh. 170,000.

Ilidaiwa kuwa, baada ya msichana huyo kuiba fedha na vitu hivyo, alikimbilia wilayani Lushoto lakini alikamatwa baadaye na kufikishwa katika kituo hicho cha polisi.

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents