Polisi Arusha watuma salamu za vitisho kwa Uhamiaji
Uhamiaji ni bingwa mara tatu wa mashindano hayo yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Sheik Amri Abeid, ambapo mkoa wa Arusha utawakilishwa na timu tatu za Polisi, Madini na Arusha City Queens.
Kocha wa Polisi Arusha, Emerciana Silas amesema nafasi ya wenyeji waliyopewa wataitumia vizuri kuhakikisha ubingwa unabaki hapo ili kuonyesha klabu zingine za mikoani kutoa fikra kuwa kombe hili si la mkoa wa Dar es Salaam
“Mwaka huu sisi ndio wenyeji na tunataka kuonyesha wenyeji wetu kwa timu tutakazochuana nazo kuwa tuko nyumbani na hao walioshikilia kombe miaka yote wajiandae kuliachia, niseme tu kuwa kimazoezi tuko vizuri na tunafanya hapa hapa, hivyo kwa mwaka huu hakuna jipya chini ya jua tutakalolishindwa na uzuri mbinu zao (Uhamiaji) hivyo kikubwa kwa sasa wadau wa Arusha waje washuhudie tunavyochukua kombe,” amesema Silas kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Kibira amesema wameamua kuyapeleka mashindano hayo mkoa wa Arusha ili kutoa fursa kwa timu wenyeji kujaribu bahati yao ya kupoka ubingwa wa Uhamiaji.