Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Polisi kumsaka upya muuaji wa mchora katuni aliyeuawa miaka 30 iliyopita

Polisi wa nchini Uingereza wamesema wanaanza upya kufuatilia muuaji aliyemuuwa mchora katuni maarufu nchini humo Naji al-Ali ambaye alikuwa raia wa Palestina mwaka 1987.

Mchoraji huyo ambaye alikuwa akichora katuni hizo katika gazeti la Kuwaiti ambaye alifahamika zaidi kwa kukosoa uongozi wa watawala wa kiarabu katika nchi zao kupitia michoro hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa njiani kuelekea ofisini kwake.

Polisi wamedai kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na watu ambao hawakutaka kuzungumza wakati mauaji hayo yalipotokea kipindi hicho pengine kwa sasa wataweza kuzungumza chochote.

Marehemu alifariki akiwa na umri wa miaka 49 na kuacha watoto wanne akiwemo Khaled, Osama, Judy na Layal. Hii hapa chini ni baadhi ya michoro ya katuni ambayo Naji al-Ali aliwahi kuichora enzi ya uhai wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW