Habari

Polisi kuwashughulikia wanaoosha vioo vya magari barabarani

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema bado linaendelea na operesheni ya kuwakamata vijana wote wanaoosha vioo vya magari barabarani.

Kamanda wa kanda hiyo Lazaro Mambosasa amekiambia kituo cha runinga cha Azam kuwa ameshatoa maelekezo kwa makamanda wa wilaya za Kinondoni na Ilala ambapo tabia hiyo imearudi tena.

“Wale watoto walianza kama wanataka kutengeneza ajira lakini kundi lile kimsingi linaanza kuchipuka likiwa na viashiria vya kuingia kwenye kundi la waalifu kwa sababu wanafanya vile bila ridhaa ya mwenye gari,” amesema.

“Nilitoa maelekezo kwa makamanda wa mikoa yote mitatu lakini shida kubwa ipo Kinondoni na Ilala, kwa hiyo nilielekeza kuwa kila wakati waweka askari katika maeneo hayo kuhakikisha vijana hawa wanakamatwa,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents