Habari

Polisi nchini Ethiopia imesema imegundua kaburi la watu wengi lililokuwa na miili ya watu takriban mia mbili

Polisi nchini Ethiopia imesema imegundua kaburi la watu wengi lililokuwa na miili ya watu takriban mia mbili

Polisi nchini Ethiopia imesema imegundua kaburi la watu wengi lililokuwa na miili ya watu takriban mia mbili karibu na mpaka kati ya majimbo ya Oromia na Somali. Mamia kwa maelfu ya watu wameyahama makazi yao katika kipindi cha mwaka uliopita kutokana na ghasia katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti ya iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la FANA nchini Ethiopia, polisi imegundua kaburi hilo la watu wengi wakati ikifanya uchunguzi juu ya madai ya ukatili yaliyofanywa na Rais wa zamani wa Ethiopia katika mkoa wa Somali.

Abdi Mohammed alilazimika kujiuzulu nafasi ya Urais wa eneo hilo, August mwaka huu na kushikiliwa kifungoni akisubiri hukumu dhidi ya madai hayo, ya kuchochea mapigano ya kikabila karibu na mpaka wa Somalia na mikoa ya Oromia.

Kikosi cha polisi kinachojilikana kama Liyu kinadaiwa kufanya mauaji huku wakimpa taarifa Rais wa eneo hilo.Polisi kwa sasa wanajaribu kuitambua miili hiyo mia mbili iliyogunduliwa katika kaburi la pamoja.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents