Michezo

Polisi nchini Marekani wataka DNA ya Cristiano Ronaldo kuchunguzwa, kufuatia madai ya ubakaji

Polisi mjini Las Vegas wametoa waranti ya kuchunguzwa kwa chembe chembe za vinasaba au DNA ya Cristiano Ronaldo kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubakaji dhidi ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno anayechezea klabu ya Juventus.

Kwa mujibu wa BBC, Wakili, Peter S. Christiansen, ameiambia BBC Michezo kuwa ombi hilo ”ni la kawaida”.

Jarida la Wall Street limeripoti kuwa waranti hiyo imewasilishwa hivi karibuni katika mfumo wa mahakama ya Italia.

Ronaldo amekanusha kwamba alimshambulia mwanadada Kathryn Mayorga katika mgahawa mmoja mjini Las Vegas hotel mwaka 2009.

”Bwana Ronaldo amekua akishikilia usemi kuwa yale yaliyotokea Las Vegas mwaka 2009 ni mambo ya watu wawili waliyokubaliana, kwa hiyo bila shaka chembe chembe za DNA zitapatikana, kwa hiyo sioni haja ya polisi kutoa ombi hilo kama sehemu ya uchunguzi wao,”ilisema taarifa ya Christiansen.

Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani ambalo lilikuwa la kwanza kuangazia taarifa hiyo mwezi Oktoba, lilisema kuwa Bi Mayorga aliandikisha ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya kufanyika kwa tukio linalodaiwa.

Der Spiegel lilisema kuwa mwaka 2010, Mayogra aliafikiana na Ronaldo kutatua suala hilo nje ya mahakama ambapo alilipwa dola 375,000 ilisizungumza hadharani madai hayo.

Mawakili wake sasa wanahoji kuwa makubaliano hayo hayakuwa rasmi.

Wakili wa Ronaldo amewahi kusema kuwa mteja wake hakukataakutia saini makubaliano hayo “sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo zimepotoshwa”.

Aliongeza: ”Hatua hiyo haimaanisha amekiri kuwa na makosa.”

Bi Mayorga alipata ujasiri wa kuzungumzia masaibu yake kutokana na kampeini ya #MeToo movement, ambayo imekuwa ikiendeshwa mtandaoni.

Wakili wake amesema kuwa mteja atamfungulia mashtaka Ronaldo nchini Marekani.

Ronaldo alihamia Juventus kutoka Real Madrid mwezi Julai kwa kima cha euro 99.2.

Ameshinda tuzo ya Ballon d’Or – ambayo hupewa mchezaji bora wa soka duniani – mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 and 2017.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno aliwahi kupinga madai dhidi yake kama “taarifa ghushi” na baadae mwezi Oktoba akatoa taarifa kupitia mtandao wake wa Twitter ambapo alipinga “vikali” suala hilo.

Wakili wake anadai kuwa stakabadhi za uchunguzi zilizotumiwa na gazeti la Der Spiegel ”ni za kubuniwa” lakini gazeti hilo linasema “halina sababu” ya kutilia shaka uhalisia wake.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents