Habari

Polisi nchini Uganda waizingira nyumba ya Bobi Wine wakimzuia kwenda kwenye Tamasha, Yeye afunguka haya

Polisi nchini Uganda waizingira nyumba ya Bobi Wine wakimzuia kwenda kwenye Tamasha, Yeye afunguka haya

Maafisa wa polisi nchini Uganda wamefutilia mbali tamasha la mbunge wa Kyadondo mashariki Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine lililotarajiwa kufanyika karibu na mji mkuu wa Kampala.

Naibu inspekta jenerali wa polisi Asuman Mugyenyi anasema kwamba waandalizi wa tamasha hilo walishindwa kuweka usalama uliohitajika, kulingana na chombo cha habari cha Nile Post.

Alidai ukosefu wa mipango ya matibabu, udhibiti wa idadi ya watu na usalama kama baadhi ya maswala yaliowashinikiza kulifuta tamasha hilo.

Tamasha hilo lilikuwa liingiliane na siku ya Uhuru inayoadhimishwa Jumatano katika wilaya ya mashariki ya Siroko.

Mgombea huyo wa urais ni mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni na anajionyesha kuwa mpiganiaji wa masikini.

Aliambia waandishi wiki iliopita kwamba tamasha hilo litaendelea kama lilivyopangwa licha ya maafisa wa polisi kushindwa kujibu barua ilioandikwa ikiomba kuandaa tamasha hilo.

Kufutwa kwa tamasha hilo kunajiri baada ya marufuku ya serikali kuhusu uvaaji wa kofia ya rangi nyekundu na raia, nembo ambayo Bobi Wine amekuwa akiitumia katika vuguvugu lake la nguvu za raia.

Chini ya sheria mpya iliotangazwa mwezi uliopita, kofi hiyo kwa jina Red Beret inafaa kuvaliwa na jeshi la – UPDF.

Mwanamuziki huyo aliyebadilika na kuwa mwanasiasa amechapisha picha katika mtandao wake wa twitter akionyesha maafoisa wa polisi walioizunguka nyumba yake , mbali na vizuizi vilivyowekwa katika barabara iliokuwa ikielekea katika nyumba yake.

Pia alidai kwamba maafisa wa polisi walizunguka mali ya ya One Love Beach Busabala , ambalo ndio eneo la Tamasha hilo.

UgandaHaki miliki ya pichaAFP

Nyota huyu wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, na anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.

Alizaliwa 12 Februari 1982, Bobi Wine na alikuwa na miaka minne pekee Museveni alipoingia madarakani mwaka 1986.

Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu.

Alilelewa katika mtaa duni wa Kamwokya kaskazini mashariki mwa Kampala na alianza kujihusisha katika muziki mapema miaka ya 2000.

Nyimbo zake za mtindo wa dansi za ‘Akagoma’ na ‘Funtula’ zilikuwa maarufu sana miongoni mwa vijana.

Ana shahada ya muziki, dansi na uigizaji kutoka Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alihitimu mwaka 2003.

Aprili 2018 alifuzu na stashahada ya masuala ya kisheria kutoka Kituo cha Maendeleo ya Sheria, Kampala.

Alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka 2017 wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.

Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).

Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.

“Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki…Ninataka siasa zitulete pamoja… jinsi muziki ufanyavyo.”

Ufuasi wa Vijana

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa miaka mingi Yoweri Museveni.

vijanaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBobi Wine anajiita “Ghetto President” na anaungwa mkono zaidi na vijana

“Chama chake kitawaza iwapo sasa huu ni msururu. Bobi Wine sasa amemshinda Museveni na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye mara nne” katika uchaguzi mdogo.

“Bobi amepata ufuasi kwa nemba yake ya ‘nguvu za watu’, na ananuia kushinikiza na kupanga liwe vuguvugu,” anaongeza.

Mchambuzi wa kisiasa Robert Kirunda anasema mvuto wa Wines unatokana na kuwepo ‘pengo la uongozi’ Uganda.

“Kuna vijana wengi Uganda ambao hawana haja ya kujua vita vya kihistoria vilivyoiingiza NRM uongozini, au ukaidi wa upinzani mkuu. Wengi wanataka ajira na wanahisi uchumi hauwasaidi.”

Kirunda anasema Wine ‘anapigia upatu sana’. “Anaweza kushinikiza watu pakubwa, lakini bado hajapata nguvu kama alizonazo Besigye katika upinzani”.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents