Burudani ya Michezo Live

Polisi wa Texas waomba msamaha baada ya kumuongoza mtu mweusi kwa kumfunga kamba

Polisi wa Texas wameomba msamaha baada ya picha ya maafisa weupe wawili wakiwa wamepanda farasi wakiongoza mtu mweusi aliyeonekana amefungwa kwa kamba hatua iliyozusha ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mkuu wa Polisi wa Galveston, Vernon Hale alisema Jumatatu mbinu hiyo ilikuwa inakubalika katika baadhi ya matukio, lakini kwamba “maafisa hawakufanya uamuzi mzuri katika tukio hili”.

Alisema hakuna “nia mbaya” na imebadilisha sera ya idara “kuzuia utumiaji wa mbinu hii”.

Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wamesema picha hii imeibua mawazo kuhusu nyakati za utumwa.

Kulingana na habari iliyotolewa kutoka kwa Idara ya Polisi ya Galveston, maafisa hao wawili kwa majina P Brosch na A Smith, walimkamata Donald Neely baada ua kukiuka sheria.

Polisi walifafanua kwamba hakufungwa na kamba, lakini “alikuwa amefungwa pingu mikononi na kamba ilikuwa imefungwa kwenye pingu.

Idara iliongeza: “Tunaelewa maoni hasi kuhusu hatua hii na tunaamini maoni haya yanafaa kabisa kukomesha utumiaji wa mbinu hii.”

Kundi la watumwa wakiwa wamefungwa cheni kwa pamoja wakiongozwa na watu weupeHaki miliki ya pichaSMITH COLLECTION/GADO/GETTY IMAGES

Bwana Hale aliomba msamaha kwa Bw Neely kwa “kudhalilishwa”.

Aliongeza maafisa “wangeweza kungoja usafiri katika eneo la kukamatwa”.

“Tumebadilisha mara moja sera ya kuzuia matumizi ya mbinu hii na tutaangalia mafunzo na taratibu zote zilizowekwa kwa njia sahihi zaidi,” mkuu wa polisi alisema.

Bwana Neely yuko huru kwa dhamana lakini hakuweza kupatikana kwa ajili ya kutoa maoni, Jarida la Houston liliripoti.

Leon Phillips, mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Kaunti ya Galveston , aliiambia BBC picha ambayo ilisambaa mitandaoni ilipigwa na mtu ambaye hakutaka kufahamika.

Bwana Phillips alisema tukio hilo ni “gumu kulizungumzia” kama mkazi wa Galveston.

“Hili lilikuwa kosa la kijinga,” alisema. “Ninachojua ni kwamba kama angekuwa mzungu, wasingetumia mbinu hiyo waliotumia kwa Neely.

Alibainisha kuwa Bwana Neely ni mgonjwa wa akili, na maafisa walipaswa kungojea bila kujali ni muda gani gari ingechukua kufika, kwani “si kana kwamba wanalipwa na baada ya kukamata”.

Bwana Phillips alisema amepanga kutoa ombi la wazi katika ukumbi wa jiji ili kuangalia sera za utekelezaji wa sheria.

“Mkuu wa polisi anasema hawakuvunja sera yoyote, lakini ni sera gani ya kusafirisha mfungwa?

“Ninajuaje kuwa sera hiyo haikuandikwa mnamo 1875? Kuna maswali mengi ambayo hayajajibiwa.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW