Siasa

Polisi wa Uganda walivyoizingira hoteli ya Bobi Wine (+ Video)

Police nchini Uganda wameizingira hoteli ambayo mgombea wa urais nchini humo Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, katika mji wa Hoima magharibi mwa Uganda ambako ndiko alipo na maafisa wake wa kampeni.

Bobi ametuma ujumbe wake wa twitter akisema kuwa alilazimika kutumia njia ndefu kufika mjini humo baada ya wanajeshi kufunga barabara ambayo alitarajia kutumia.

“Wametufuata kwenye hoteli yetu na kuizingira ,” alitweet.

Televisheni ya Uganda NTV alitweet ujumbe kuwa ” lengo la operesheni hiyo bado halijajulikana “.

Bobi Wine alituma picha za polisi wakiwa nje ya hoteli alimokuwa:

Gazeti la Uganda Daily Monitor lilitweet kuwa Bobi Wine alikuwa amekataliwa kuingia katika mji huo ambako alikuwa amealikwa kama mgeni katika kipindi cha redio.

Wagombea katika uchaguzi ujao wameambiwa wafanye kampeni zao kwa njia ya vyombo vya habari na kuepuka mikusanyiko mikubwa ya watu kwasababu ya virusi vya corona

Wiki iliyopita Bobi Wine alikamatwa kwa kukiuka sheria za kuzuwia virusi vya corona.

https://www.instagram.com/tv/CIDfAfahjmy/

https://www.instagram.com/tv/CIDfAfahjmy/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents