Habari

Polisi wabaini watu 13 waliofungiwa vitandani kwa minyororo

Katika Jiji la California nchini Marekani Polisi wamebaini kuwepo kwa watu 13 waliokuwa wamewekwa kifungoni katika nyumba yao kwa kufungwa na minyororo wakiwa katika vitanda vyao.

Tukio hilo liligundulika siku ya Jumapili wakati mmoja wa watu hao alipofanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura ndipo polisi walipofika katika nyumba hiyo na kuwatia nguvuni wazazi wa watu hao na watu wengine.

Waliokamatwa ni pamoja na David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, wote kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.

Msichana mwenye umri wa miaka 10 ambaye ndiye alitoa taarifa polisi alidai kuwa ndegu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao, hata hivyo baadaye polisi walikuta watoto kadhaa wakiwa wamefungiwa katika vitanda na minyororo katika mazingira yenye harufu mbaya na giza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents