Habari

Polisi wadaiwa kumvunja raia, wambambikizia kesi

Mtuhumiwa anayedaiwa kuvunjwa miguu na mikono na polisi wa Kituo cha Katoro, wilayani Geita amelalamikia kile alichodai polisi wamembambikizia kesi tofauti na makosa yake.

David Azaria, Geita


Mtuhumiwa anayedaiwa kuvunjwa miguu na mikono na polisi wa Kituo cha Katoro, wilayani Geita amelalamikia kile alichodai polisi wamembambikizia kesi tofauti na makosa yake.


Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Geita, Zablon Kesase ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Msaidizi wa Polisi Thomas Mboya kwamba Magire Sitta (33) alivunja mahabusu ya kituo cha Polisi cha Katoro baada ya kufanya vurugu katika kituo hicho, kumpiga mtu mmoja ambaye hata hivyo Mtuhumiwa Magire Sitta (33) anayedaiwa kuvunjwa miguu na mikono kwa kupigwa na polisi wa Kituo cha Polisi Katoro wilayani Geita mkoani Mwanza, akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu. (Picha na David Azaria).jina lake halikutajwa, Machi 30 mwaka huu na kutishia kuua mtu ambaye naye hakutajwa.


“Hakimu hawa polisi nadhani wameanza kutapatapa kwa sababu hata kosa nililokamatiwa sijasikia limetajwa kwenye mashitaka yote matatu.
“Mimi nilikamatwa kwa madai kwamba nimemtorosha hawara wa askari ambaye tulikuwa tunakunywa naye bia kwenye baa tukiwa na askari huyo.


“Waliponifikisha kituoni wakaanza kunipiga hadi kufikia hatua hii. Sasa nashangaa kusikia mara nimempiga mtu mwezi wa tatu…mara nimetishia kumuua mtu..” alilalamika mtuhumiwa mbele ya hakimu.
“Kama ni hivi ni bora walete bunduki ili wanipige risasi nife tu kwa sababu sina hata faida tena hapa duniani. Wamenivunja miguu yote kama unavyoiona, mikono yangu…halafu bado wananibambikizia kesi hivi kweli haki ipo hapa nchini…? aliuliza.


Mwananchi huyo alisomewa mashitaka hayo mwishoni mwa wiki, huku akiwa hoi kitandani katika wodi ya majeruhi ya Hospitali ya Wilaya ya Geita.


Sitta alikana mashitaka yote na alinyimwa dhamana kwa madai kwamba upelelezi wa mashitaka yake haujakamilika.


Katika hatua nyingine askari wawili wanaotuhumiwa kumpiga hadi kumvunja miguu na mikono mwananchi huyo wanahojiwa na Polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Athur Magoti alithibitisha kushikiliwa kwa askari hao kuhusiana na tukio hilo. Alisema itatolewa taarifa kuhusu suala hilo.
Mara kadhaa HabariLeo iliwashuhudia askari hao wakizungumza na majeruhi huyo kwa kumhamishia chumba maalumu wodini alikolazwa kwa ajili ya mazungumzo ya mwafaka, huku wakimweleza kwamba endapo atakubali kuwasamehe wako tayari kumfutia mashitaka waliyomfungulia.
Baadhi ya ndugu zake wamethibitisha kuwa askari hao wamekuwa wakitafuta suluhu juu ya suala hilo.
Hata hivyo ndugu hao wamesema hawako tayari kuwasamehe kwa kile wanachokielezea kwamba ni unyama mkubwa waliomtendea ndugu yao ambaye hata kama atapona atakuwa na kilema cha maisha.


‘Wao siyo wastaarabu kama walijua kwamba hana kosa kwa nini wamembambikizia kesi hizo zote. Wao walianza kufanya lakini sasa sisi tunamalizia, hatuko tayari kutafuta mwafaka wakati wamefanya unyama wa namna hii,” alisema kaka wa majeruhi huyo, Lwissa Sitta.


Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents