Michezo

Polisi wagoma kukisindikiza kikosi cha Man United, Mourinho aipongeza UEFA na mwamuzi kwa huruma yao

Klabu ya Manchester United kwa sasa inapitia misukosuko mbalimbali ndani na nje ya uwanja ukilinganisha na miaka mingine iliyopita na hili limejidhihirisha hapo jana kuelekea mchezo wao wa UEFA Champions League dhidi ya Valencia waliotoka sare ya 0 – 0.

Kuelekea mchezo huo katika hali isiyo ya kawaida kikosi cha Man United kimejikuta kikichelewa kutoka ndani ya hoteli kufika kwenye uwanja wao wa Old Trafford uliyopo umbali wa maili tatu sehemu ambayo mechi hiyo ilipangwa kuchezwa baada ya polisi wa jiji la Manchester kukataa kukisindikiza ‘escort’ kikosi cha mashetani hao wekundu na hivyo kuchelewa njiani.

Mourinho alijikuta akiwa mwenye hasira baada ya kuchelewa kuondoka Lowry Hotel ambapo ilichukua dakika 75 kuelekea kwenye uwanja wa Old Trafford na kufika majira ya saa 7.15 pm badala ya 6pm kama ilivyokusudiwa jambo ambalo limechangia wachezaji kukosa muda wa kutosha kupasha misuli ‘warm’ kabla ya kuwakabili Valencia.

Hali hiyo imepelekea mchezo huo kuongezwa dakika tano na hivyo kuchezwa 8.05pm huku wachezaji wa Manchester United kukosa muda wa kutosha kujiandaa kabla ya mechi.

“Tuliondoka hotelini saa sita tukiamini kuwa dakika 30 zingetutosha kitu ambacho ni kawaida, lakini safari hii polisi wamekataa kutusindikiza ‘escort’ na hivyo tumekuja wenyewe,” amesema Mourinho.

‘Tumetumia dakia 75. UEFA walikuwa waungwana, mwamuzi amekuwa muungwana pia ambapo ameturuhusu kuanza mechi dakika tano baadae kwasababu tulihitaji angalau saa moja na nusu kwaajili ya kufanya maandalizi.”

Wageni wa mchezo huo Valencia licha ya kuwa umbali wa maili sita kutoka uwanja wa Old Trafford lakini wakiwa Worsley Marriott lakini waliweza kufika kwa wakati ukilinganisha na wenyeji wao

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents