Habari

Polisi wamkamata kijana aliyetamani kuonana na Donald Trump

Homa ya uchaguzi nchini Marekani inazidi kupamba moto. Kijana wa miaka 20 amekamatwa na polisi wa Marekani akijaribu kupanda jengo lenye ghorofa 58 kwa madai ya kutaka kuonana na mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.

Polisi-Marekani-702x336

Kijana huyo anayetumia jina la Leven Thumps alililipanda jengo hilo la Trump Tower lililopo New York na alitumia kamba kupanda jengo hilo kwa muda wa masaa matatu mpaka kufikia ghorofa ya 21 ambapo polisi walimkamata.

Aidha Leven Thumps amedai kuwa amepanga kutumia kila njia ili aweze kupata nafasi ya kuonana na mgombea huyo wa chama cha Republican.

Polisi

“Niamini na kama maombi yangu yatazuiliwa, sitaweza kuhatarisha maisha yangu kwa ajili ya jambo hilo. Sababu ya kupanda jengo lako ni kutaka kila mtu afahamu dhamira yangu,” alisema kijana huyo.

Mmoja wa maafisa wa polisi wa nchi hiyo amesema kuwa walimuona kijana huyo akipanda kwenye jengo hilo ndipo wakachukua hatua ya kwenda kumuokoa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents