HabariUncategorized

Polisi wanamsaka mwanamke anayejisaidia hadharini

Polisi nchini Marekani wanamsaka mwanamke mkimbiaji ambaye amepewa jina la ‘mchafuzi kichaa’ kwa kuwa anatabia ya kijisaidia haja kubwa nje ya nyumba za watu.

Mwanamke huyo amekuwa akiacha kinyesi chake nje ya nyumba za watu kwa zaidi ya mara saba kwa wiki za hivi karibuni ,licha ya kwamba kuna vyoo vya umma karibu.

Inawlezwa kuwa watoto wa jirani walimuona mwanamke huyo wakati alipokuwa akijisaidia,akiwa amechuchumaa karibu na nyumba Colorado.

Idara ya polisi mjini humo imesema kuwa tabia ya aina hiyo ni ya “ajabu”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents