Habari

Polisi Wanne Kenya wasimamishwa kazi kwa kumpiga mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Jomo Kenytta – Video

Polisi Wanne Kenya wasimamishwa kazi kwa kumpiga mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Jomo Kenytta - Video

Jeshi la Polisi nchini Kenya limewasimamisha kazi Askari wanne walionaswa kwenye mkanda wa video wakimpiga Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia. Wanafunzi walikuwa wakiandamana kutokana na kuzorota kwa usalama chuoni hapo.

Lazima tuhukumu ukatili wa polisi kwa wanafunzi. Namaanisha kwa sababu ya Mungu huyu ni mwanafunzi sio gaidi, “Ispan Kimutai aliandika.

“Lazima pia tujiulize ni kwanini wanafunzi wa vyuo vikuu wanapaswa kukutana na nguvu kubwa kila wakati wanapokuja kuandamana,” Muthuri Kathure aliandika.

“mtu huyo ambaye alikuwa na uwepo wa akili ya kurekodi tukio hilo na [nawashukuru] Wakenya wote ambao walifanya kuwepo na ushshidi”.

Hapo awali, Bwana Mutyambai, alielezea kile kilichotokea kama “tukio la bahati mbaya”.

Maafisa wote wa polisi walikuwa “wamepata mafunzo juu ya hitaji la kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kila mtu”, alisema.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents