Habari

Polisi watakiwa kuwanyoosha watakaovunja sheria za barabarani

Naibu waziri wa mambo ya ndani, Hamad Yussuf Masauni, amelitaka jeshi la polisi na wasimamizi wa sheria kutofumbia macho wanaovunja sheria za barabara nchini ili kupunguza ajali.

mass1-768x510

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama waziri huyo, Masauni,amesema kama wananchi wakiamua kufuata sheria zilizowekwa ajali zitapungua.

“Jeshi la polisi na wasimamizi wengine wa sheria, endeleeni kuchukua hatua kali na madhubuti za kukabiliana na hali hii bila kumuogopa wala kumuonea aibu mtu yeyote. Makundi yote ya utumiaji wa barabara yana wajibu mkubwa ya kuzitumia barabara zetu, tutambue wote tuwajibike kupambana na zile ajali za barabarani, hivyo inatubidi tushirikiane, kuelekezana na kumuonya kila mmoja wetu anapovunja sheria na kanuni za usalama barabarani,” alisema Masauni.

Aidha Masauni amelitaka shirika la viwango nchini Tanzania (TBS) kuhakikisha magari na matairi yote ya nchini ili kupata bidhaa zenye ubora zitakaosaidia kupunguza ajali za mara kwa mara.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents