Habari

Polisi yawasaka walimu waliomsababishia mwanafunzi kifo

Siku moja baada ya vyombo vya habari kuripoti Kisa cha Mwalimu Mkuu kumfungia mtoto katika chumba cha hazina, mwanafunzi Daudi Kaila wa shule ya msingi Matwiga na kusababisha kifo chake, Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama wilayani humo kuwasaka na kuwatafuta walimu hao popote walipo.

Mkuu wa Wilaya huyo alipofika katika shule hiyo pamoja na kuzungumza na wananchi alitoa pole na kuwahakikishia wananchi kuwa haki itatendeka kwa yeyote aliyehusika.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana hakikisheni mnawatafuta watu hawa, hakikisheni mnawatafuta waklimu wote waliohusika kwa kushirikiana na wananchi,” alisema Madusa.

Kwa upande wa Jeshi la polisi wilayani Chunya limewaahidi wananchi kuwa haki itatendeka.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents