Habari

Presha ya Christmas: SUMATRA waruhusu daladala kusafirisha abiria Moshi na Arusha

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA wamelazimika kuruhusu magari madogo maarufu (daladala) kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo Moshi na Arusha baada ya idadi kubwa ya abiria kukosa nafasi kwenye mabasi makubwa.

Wakizungumza na ITV baadhi ya abiria waliokosa usafiri wamedai kuwa walishindwa kukata tiketi mapema kutokana na kuona hakuna tatizo la usafiri tangu mwezi huu uanze hivyo wameshangazwa na hali waliyoikuta kituoni hapo.

Kufuatia uhaba huo wa magari baadhi ya wamiliki wa mabasi wametumia fursa hiyo na kutoa mabasi yaliyokuwa karakana kwa matengenezo ambapo baada ya kufanyiwa ukaguzi na askari yakaonekana kuwa na kasoro hivyo kuzuiliwa kuendelea na safari ili hali walikuwa wameshapakia abiria.

Kituo hicho cha TV kilienda kushuhudia msongamano wa abiria huku wengine wakirudi nyumbani baada ya kukosa usafiri ambapo akizungumzia suala la kutoa vibali kwa daladala kwenda mikoani mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri wa barabara SUMATRA Johansen Kahatano amesema wamefanya hivyo ili kusaidia abiria waliokosa huduma.

Wakati huo huo Naibu kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amewatahadharisha watumiaji wa barabara kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka mahabusu kwani kamera za usalama zitakuwepo kila kona ya jiji.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents