Tupo Nawe

Prezzo afuata nyayo za Jaguar, Professor Jay na Sugu, Ajitupa rasmi kwenye siasa (+video)

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Kenya, Jackson Makini almaarufu kwa jina la Prezzo ametangaza rasmi kuingia kwenye siasa kwa kuchaguliwa nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo la Kibra nchini humo.

Prezzo ameteuliwa na Chama cha Wiper leo Jumanne Septemba 10, 2019,  mbele ya kiongozi wa Chama hicho,  Kalonzo Musyoka ambaye alishawahi kuwa makamu wa Rais wa Taifa hilo.

Taarifa hiyo imepokewa na kwa mikono miwili na Wakenya, Huku wengi wakimlinganisha na msanii mwenzie wa muziki, Jaguar ambaye yeye kwasasa ni Mbunge wa Jimbo la Starehe.

Kalonzo anaamini kuwa kutokana na ukumbwa wa Prezzo,  Anauwezo mkubwa wa kuchukua jimbo hilo kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 7 mwaka huu.

Prezzo atapambana na mwakilishi mwingine wa Chama cha ODM, Imran Okoth kwenye kinyang’anyiro cha kusaka ubunge kwenye jimbo hilo la Kibra.

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW