Picha

Prezzo na Diva watavuka milima na mabonde? Jina la Diva lasambaa kwa kasi, ‘booked for interview all over Africa now’

Prezzo anaweza kujiita mwanaume mwenye bahati kuliko wanaume wote duniani? Yeah, walau kwa sasa kwakuwa jina lake halitoki mdomoni mwa mtangazaji wa Clouds FM , Loveness aka Diva. Diva kapenda na haambiwi kitu. “Love is blind , kijana wa Nairobi kanichanganya and a tat will do me good. for better for worse his name will be in ma heart,” ametweet Diva kueleza penzi motomoto alilonalo kwa mfalme wa bling bling, Prezzo.

09257534b8b311e2b1f822000a1f9751_7

Prezzo ana bahati kwakuwa Diva amempiga chini mpenzi wake kwa sababu yake. “My Baby… he makes me happy and it was truely love at first sight.. now am thinking like a man.. Dumping my man over Prezzo .. for sho.”

Japokuwa uhusiano wao ambao haujamaliza hata wiki tangu ujulikane hadharani, tayari umekuwa gumzo katika nchi zote mbili, Kenya na Tanzania, na sasa nchi zinaanza kutekwa na habari hii. Tayari Diva ameshapata mashemeji na mawifi wa Kikenya japo sio wote wanaofurahia uhusiano wao mpya.

Jana Diva alijikuta akiingia kwenye vita vya maneno na model mwenye maneno lukuki, Huddah Monroe. Vita hivyo vimezalisha makundi mawili yanayotupiana vijembe, Team Diva na Team Huddah. Diva anasema Prezzo ni mpenzi aliyetoka juu mbinguni, ‘sent from above’ na leo amepanga kwenda kujichora tattoo kudhihirisha ni kwa kiasi gani anampenda. “Getting ready going to my tattoo artist, all I need is PREZZOO name in my heart. Love Love Love ♥. I wanna have him in me, I so need his name in my heart, want him to live forever and ever.”

Kwa wanaomfahamu Diva, haya anayoyafanya leo si mageni. Ndivyo alivyo akipenda. Watu wengi waliufahamu uhusiano wake na rapper Mo Rocka. Diva alikuwa akimtaja karibu kila siku kwenye kipindi chake cha Ala za Roho. Jinsi walivyoagana jana, jinsi alivyomkiss na mambo mengine ya faragha. Kwake Diva hicho ni kitu cha kawaida, kashapenda, humwambii kitu. “I’m very much in love and that is one thing for sure. God Is Good. Kenyan Sweetest Prezzo have my heart,” ameendelea kusisitiza mahaba mazito kwa Prezzo.

Leo hii wakenya ambao walikuwa hawamfahamu Diva, wamemfahamu katika kipindi kifupi tu. Jina lake limegusa vichwa vingi vya habari vya mitandao na magazeti ya Kenya na kwingineko. Hii ni mifano ya headline zilizoandikwa kwente website za Kenya:

Prezzo Dating a Tanzanian Damsel, Planning to Get Married (Ghafla)

Prezzo in a denied Love Again With DIVA AKA Loveness Love (Malimwengu)

Photos of Prezzo’s New Tanzanian Girlfriend (Nairobi Wire)

Prezzo Dating Tanzanian Girl Diva (kenyanlist)

Na kuonesha jinsi gani habari hiyo imesambaa, Diva ametweet: booked for interview all over Africa now.”
Kwa kazi ya Diva, uhusiano wake na Prezzo unaweza kumfikisha mbali. Kama akiendelea na spidi aliyonayo sasa, ni rahisi kupata kazi kwenye vituo vikubwa vya radio ama runinga.

“Been so happy lately… and am like all over Big Brother Africa social Network. All over Kenya and Am all over Africa,” anasema Diva.

Swali ni Je! Prezzo na Diva watavuka milima na mabonde? Hii ni kwasababu kwa wengi uhusiano huu unaonekana kama wa kuigiza tu.

“She sounds insane and out of her mind,what does being all over Kenya and Africa got to do? Sorry for the person who got dumped,” ameandika follower wake wa Instagram.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents