Burudani

Prince Harry awaalika maex wake kwenye harusi yake na Meghan Markle mwezi Mei

Ukiwa unafunga ndoa, unaweza ukamualika ex wako? Prince Harry ameripotiwa amewalika wapenzi wake wawili wa zamani kwenye harusi yake na Meghan Markle inayotarajiwa kufanyika Mei 19 ya mwaka huu.

Prince Harry amewaalika Cressida Bonas na Chelsy Davy. Hilo limethibitishwa na mtu wa karibu wa Harry alipokuwa akiongea na mtandao wa Daily Mail.


Picha ya Prince Harry akiwa na Chelsy Davy enzi za mahusiano yao

“Harry amekuwa na urafiki mzuri na Chelsy na Cressida, kwa hiyo watakuwepo. Alihakikisha kuwa hakuwa na hisia ngumu wakati waligawanyika. Sidhani Meghan atachukia,” kimesema chanzo hiko.


Prince akiwa na Cressida Bonas wakati wa mahusiano yao

Cressida Bonas aliwahi kuwa na mahusiano na Harry kwa miaka miwili, wakati Chelsy Davy walidumu kwenye mahusiano wa muda wa takriban miaka saba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents