Burudani ya Michezo Live

Prince Harry na Meghan ruksa kujitegemea, atarajia kulipa zaidi ya bilioni 70 za Kitanzania

Kasri la Buckingham limetangaza rasmi kuwa Prince Harry na mkewe Meghan hawataruhusiwa tena kutumia vyeo vya kifalme walivyonavyo na hawatapokea tena fedha za Umma kwaajili ya shughuli za kifalme.

Image may contain: 2 people, people smiling

Mbali na hayo wawili hao pia hawatahusika tena na shughuli za kumwakilisha Malkia.

Aidha taarifa hiyo pia imeongeza kuwa watawala hao wa Sussex watatakiwa pia kulipa paundi milioni 2.4 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 70 kama kodi kwaajili ya marekebisho ya makazi yao ya Frogmore Cottage ambayo yatakuwa nchini Uingereza.

Makubaliano hayo mapya yanatarajiwa kuanza rasmi mwezi Machi mwaka huu, kwa mujibu wa taarifa ya kasri.

Taarifa hiyo imekuja kufuatia mazungumzo yaliyofanyika mwanzani mwa juma hili kati ya Malkia na wawili hao kuhusu hatma ya maisha yao ya baadaye baada ya kutangaza kuwa wanataka kujitoa katika majukumu ya kifalme na kufanya shughuli zao kwa kujigawa kati ya Uingereza na Canada.

Image may contain: 2 people, people standing and beard

Katika sehemu ya taarifa hiyo Malkia amenukuliwa akisema ” kwa miezi kadhaa ya majadiliano na mazungumzo mengi ya hivi karibuni” nimeridhia” kwa pamoja kupatikana kwa suluhisho lenye kujenga na kusaidia namna ya kumwezesha mjukuu wangu na familia yake”.

“Harry, Meghan na Archie watakuwa wakati wote ni wajumbe wanaopendwa katika familia yangu ya kifalme,” iliendelea kueleza taarifa hiyo.

Amewashukuru kwa “kazi walizojitoa”, na kuongeza kuwa alikuwa “akijivunia namna Meghan alivyojitahidi kwa haraka kuwa mmoja wa wanafamilia.”

Lakini kwa upande wa wachambuzi wa mambo akiwemo Katie Nicholl, mwandishi wa kujitegemea wa jarida la Vanity Fair anayeandika masuala ya Kifalme amesema, kujitoa kwa Harry na Meghan katika shughuli za kifalme ni pigo kwa taasisi hiyo maarufu ulimwenguni.

“Watawala wa Sussexes wameshinda kwasababu wamepata walichotaka, ambacho ni Uhuru kutoka Faimilia ya Kifalme. Harry na Meghan wameweza kuleta maajabu na upekee kwa familia ya kifalme,” alisema Nicholi.

Amesema makubaliano hayo pia yanaweza kufungua njia kwa vijana wa kizazi cha sasa wa kutoka familia za kifalme katika miaka ijayo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW