Burudani

Producer Elly da Bway aamua kuimba baada ya kudai nyimbo nyingi sokoni zinafanana (Video)

By  | 

Mtayarishaji wa muziki nchini, Elly da Bway kutoka studio za Home Town Records amefunguka sababu ya kuamua kuingia kwenye kuimba kama alivyotangaza wiki iliyopita.

Akiongea na Bongo5, Elly amesema, “Nimeamua hivyo ili niweze kufanya na mimi, kwa sababu kuna vitu ambavyo naona vimemiss Kwenye vocals, kwa hiyo nataka kuviweka sawa. Nimekuja na vitu tofauti, nimekuja na style tofauti kidogo ya uimbaji, kwa hiyo kitu ambacho ninakihitaji ninaomba watu wakae tayari kumsikiliza Elly da Bway anakuja na kitu gani.”

Akiongelea vitu ambavyo alivyonavyo vya utofauti na wasanii wengine, mtayarishaji huyo amesema, “Kitu cha kwanza ni kwenye upande wa idea, kitu cha pili ni nyimbo yenyewe ambapo mtu akisikiliza anapata kitu kile ambacho sio alichokizoea siku zote. “Kwa mfano, sasa hivi ukikaa kwenye redio ukisikiliza nyimbo nyingi unaweza ukasema ni nyimbo moja au zimefanywa na mtu mmoja. Kwa hiyo nimejaribu kufanya kitu cha tofauti kuonyesha watu kuna vitu kama hivi pia vinaweza vikafanyika na hiki kinaweza kikafanyika ili watu waweze kubadilika kidogo tusifanye kitu kile kile kila siks.”

Muimbaji huyo anatarajia kuachia rasmi wimbo wake wa kwanza uitwao ’Boss’ wiki ijayo ambao pia ameutayarisha yeye mwenyewe huku video yake ikiongozwa na Mims.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments