Burudani

Producer Elly da Bway kufuata nyayo za Nahreel

Elly da Bway ameamua kufuata nyayo za Nahreel, Mesen Selekta, Nuh Mziwanda na wengine kwenye muziki.

Mtayarishaji huyo wa muziki kutoka studio ya Home Town Records ameamua kuingia kwenye muziki kama msanii na wiki ijayo anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao ameutayarisha mwenyewe.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Elly amesema, “Tayari nina nyimbo kadhaa, lakini wiki ijayo nitaachia wimbo wangu wa kwanza na kuanzia Jumamosi nitaanza kushoot video ya wimbo huo. Director atakuwa ni Mims kwa kuwa ni mmoja ya madirector ninaowakubali zaidi hapa nchini.”

“Bado nitakuwa naendelea na utayarishaji wa muziki kama kawaida, lakini nitakuwa nikiachia kazi zangu kwa kuwa ni kipaji kingine ambacho ninacho. Tayari nimewahi kuandikia nyimbo wasanii na zikafanya vizuri,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents