Tupo Nawe

Producer Jermaine Dupri hatarini kupoteza haki za nyimbo za label yake ya ‘So So Def’

Madeni madeni madeni!! Kirusi cha ‘Deni’ kimeonekana kuwasumbua wanamuziki wengi maarufu duniani siku za hivi karibuni. Baada ya Mary J. Blige na Lauryn Hill kuripotiwa kupata virusi hivyo vilivyokosa ‘anti-virus’, sasa maambukizi yamehamia kwa producer na rapper mkongwe Jermaine Dupri.

jermaine-dupri

Mwanzilishi huyo wa label ya So So Def ya Atlanta, Georgia, Marekani iliyowatoa wanamuziki wakubwa kama Bow Wow yuko katika hatari ya kupoteza haki za nyimbo za wasanii wa label yake, kutokana na kushindwa kulipa deni kubwa la mkopo aliochukua.

Deni hilo linatokana na mkopo wa dola milioni 4.8 aliouchukuwa kutoka Sun Trust Bank mwaka 2010, ambao alifanikiwa kulipa zaidi ya nusu ya deni hilo. Kwa mujibu wa TMZ, baada ya Dupri kuacha kumalizia kulipa deni hilo benki hiyo ya Trust imelazimika kumfungulia Dupri mashitaka ya deni la karibia $ 2M iliyobaki pamoja na riba.

Hatari iliyopo katika kesi hii ni kuwa wakati Dupri anataka kuchukua mkopo aliweka hati miliki na mirahaba (royalties) za nyimbo nyingi zinazomilikiwa na label hiyo, zikiwemo za wasanii kama Bow Wow, Da Brat na Xscape.

Hii ni kama episode mpya ya matukio ya madeni kwa producer huyu baada ya mwezi wa pili mwaka huu alifanikiwa kulipa deni la kodi lililofikia dola milioni tatu lililodumu toka 2006, na mwaka jana alifanikiwa kuokoa jumba lake kutokupigwa mnada kwa mara ya pili mfululizo kutokana na madeni.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW