Burudani

Producer Lucci (TransforMax Recs) atangaza ofa ya wimbo na video kwa waimbaji wawili wa kike

Producer wa hit ya Ben Pol, Jikubali, Lucci Tsere aka Lucci Da Don ametengaza ofa ya wimbo na video kwa wasichana wawili wakali.

60720_394134850687940_1240323705_n

“Nina nyimbo mbili za kutoa bure kuanzia production, hadi lyrics, hadi video…ila kwa mwanadada tu,”aliandika kwenye Twitter.

Bongo5 imezungumza na Lucci kutaka kufahamu zaidi ofa hiyo ikoje ambaye amesema anahitaji wasichana wanaovutia, wenye sauti nzuri na wanaoweza kuongea Kiingereza.

“Attractive, very attractive, kama she is under 18 awe na ruhusa kutoka wa wazazi wake and it should be signed between me and them. Awe na sauti nzuri na mwenye uwezo kiasi kuongea Kiingereza kwa maana ya tone yake ya sauti iwe international. Mfano mzuri wa tone ya Maua. Awe na character inayofundishika na we msikivu akiwa anapewa maelekezo,” amesema Lucci kwenye maelezo aliyoipa Bongo5.

Lucci amesema kwa wasichana wanaotaka kupata shavu hilo wawasiliane naye kwa email: [email protected].

“Watume picha na wakitaka advantage zaidi watume na audio clip if possible. Lasivyo after email watapewa physical appointment, watakuja ofisini kwangu Kida Plaza, Mikocheni,” ameongeza.

Wakati huo huo Lucci amesema anatarajia kuachia single yake mpya iitwayo Sumu.

Unaweza kulike page ya Facebook ya TransforMAX Records HAPA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents