Producer mahiri wa muziki Ensayne Wayne, amepigwa risasi na kuuawa

Producer wa muziki Ensayne Wayne amepigwa risasi na kuuawa katika jiji la Atlanta jana usiku (Februari 10). Ensayne alikuwa kaka mkubwa wa Producer maarufu Drumma Boy na wawili hao walikuwa wakitengeza midundo mizuri wakiwa pamoja.

Ensayne Wayne (kushoto) akiwa na mdogo wake Drumma Boy (kulia)

Ensayne ametengeneza midundo mbalimbali kwa wasanii kama Three 6 Mafia, 8Ball & MJG, Jeezy, Future, Young Buck, Xzibit na wengine wengi. Pia Ensayne Wayne na Drumma Boy walishikirikiana katika kutengeneza biti la muziki uitwao “Shwaty” wa Plies aliomshirikisha T-Pain na muziki huo uliweza kushika nafasi ya 10 katika chati za Billboard Top 10 hit Shawty.

Fox5 inaripoti kuwa tukio hilo lilitokea katika duka liitwalo “The House of Fresh” ambalo ni duka la nguo la Drumma Boy liliopo huko jijini Atlanta. Ensayne Wayne alipigwa risasi ya kifua baada ya kushiriki katika shambulio hilo la bunduki kwa sababu ambazo bado hazijajulikana. Ensayne alikuwa akibeba bunduki pia.

Hakuna risasi nyingine zilizoingia ndani ya duka na hakuna mtu mwingine aliyeumia katika tukio hilo. Mtuhumiwa huyo inasemekana kuwa aliondoka na gari lenye rangi ya silva, kwa mujibu wa polisi wa Atlanta ambao bado wanatafuta uchunguzi zaidi. Na wameeleza kuwa mtuhumiwa ni mwanamume mwenye rangi nyeusi.

Drumma Boy alithibitisha kifo kwa kutoa ujumbe kupitia mtandao wa Instagram huku akionyesha kumbukumbu za zamani za familia yao.

Pumzika kwa amani Ensayne Wayne.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW