Habari

Producer Mbezi: Nguvu ya Hip Hop ya Tanzania imepungua kasi

Producer wa Tilalila ya Mr Blue, Desmond Deogratius aka Mbezi amesema nguvu ya hip hop ya Tanzania imepungua.

Mbezi

Akiongea kwenye mjadala maalum na Bongo5, Mbezi amesema hip hop ya sasa si kama ya zamani na imezidiwa nguvu na muziki wa kuimba. “Ukilinganisha na zamani enzi za marehemu Complex, AY , Crazy GK wa zamani na vitu kama hivyo,”amesema producer huyo.

“Siku hizi hata hip hop wenyewe naona wanahama kabisa wanaingia kwenye Bongo Flava.”

Mbezi amesema sababu kubwa ya hip hop kushuka kasi ni kutokana na vituo vya redio kutoipa muda wa kutosha hewani.

“Kipindi kikifika, kuna nyimbo fulani zinakuwa kwenye rotation zaidi kuliko nyimbo fulani. Hiyo inasababisha baadhi ya muziki upotee au uishie nguvu. Lakini kama muziki wowote mzuri ungekuwa unapigwa, naamini muziki wote ungekuwa standard na tusingekuwa tunasema Bongo Flava inalipa zaidi kuliko hip hop.”

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/128296185″ params=”color=ff6600&auto_play=false&show_artwork=true” width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents