Burudani

Producer wa Tanzania atayarisha ‘official remix’ ya wimbo wa wasanii wawili wakubwa wa Nigeria

Producer na ambaye pia msanii anayefanyia kazi kwenye studio za Upraise Music, Fraga amefanikiwa kufanya remix ya wimbo wimbo uitwao “Oga Thomas” wa muimbaji wa Nigeria, Papa ambaye pia amemshirikisha Sele Bobo.

Papa ft. Selebobo – Oga Thomas

Sele Bobo anafahamika kwa kutayarisha hits za Yemi Alade ukiwemo ‘Johnny’.

Aiongea na Bongo5, Fraga amesema alikuwa akiwasiliana na Papa katika mtandao wa Instagram ndipo wakapeana contact na kukubaliana amfanyie remix ya wimbo huo.

“Kwangu mi naona ni furaha maana hadi mtu kuniamini nifanye kazi yeake sio rahisi maana huyu dada ni msanii mkubwa huko kwao,” amesema Fraga. “Yeye na team yake walisikiliza hiyo yangu wakaipitisha kuwa itoke iwe official remix. Nadhani pia ntafanya kazi nyingine na Sele Bobo. Amependa kazi zangu maana kuna beat nimemtumia baadhi na kazi ambazo nimeshafanya kama kuna kazi mpya ya msanii wa hapa nyumbani anaitwa Asia, nadhani inatoka hivi karibuni wameipenda sana hiyo kazi nilivyoitengeneza.”

Huu ndio wimbo original wa Papa uliotayarishwa na Sele Bobo:

Na hii ndo remix ambayo imetengenezwa na producer Fraga:

1

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents