BurudaniHabari

Prof ni Prof na Rhyno ni Rhyno

Black Rhyno‘Unajua kama ni kupata mafanikio katika muziki kupitia mgongo wa Kaka yangu naamini ningekuwa mbali sana, lakini kusema ukweli hakuna msaada ninanoupata, kila ninachokifanya kwenye sanaa ni kwa jitihada zangu binafsi’-Black Rhyno.

‘UBlack Rhynonajua kama ni kupata mafanikio katika muziki kupitia mgongo wa Kaka yangu naamini ningekuwa mbali sana, lakini kusema ukweli hakuna msaada ninanoupata, kila ninachokifanya kwenye sanaa ni kwa jitihada zangu binafsi’-Black Rhyno.

Hapo awali alijulikana kama mmoja kati ya wanaounda kundi la choka mbaya ambalo mpaka sasa limebaki kuwa hadithi ambayo haijawekwa bayana na kusababisha watu kutoelewa hatma ya kundi hilo.

Akielezea kwa upande wake alipofikishana na kundi hilo alisema ‘unajua choka mbaya walipokuwa akianza kila mtu alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kundi linafanya vizuri hata mimi niiona kweli bro (Prof Jay) ameamua kutupa nafasi wadogo zake’

‘na hata Prodyuza majani alikuwa ana moyo wa ajabu kuhakikisha choka mbaya inafanya vizuri, ambapo alijitolea kwa hali na mali na kututengenezea mikono ya kweli kabisa ambayo kama tungefanikiwa kuchomoka nayo tungekuwa mbali sana’ alisema Rhyno.

Wakiwa kama choka mbaya walifikia mpaka hatua ya kurekodi mkono mmoja ambao alisalia Professa tu kuingiza sauti lakini alikuwa akizingua na matokeo yake hakuna kilichofanyika mpaka alipoamua kuimwaga project hiyo na kufanya mambo yake.

‘makuabaliano ilikuwa ni kila mtu apige mkono mmoja nikiwa mimi na mwanangu Adili, kisha ndio utaratibu wa albam ya choka mbaya uendelee, lakini nilipotoka na ngoma yangu ‘mistari’ ambayo nilisaidiwa na majani baada ya kuona choka imefeli na mchizi katumwaga kabisa hata katika show zake akawa hatushirikishi yaani kwa kifupi hakuna msaada wowote ambao tunaweza kusema jamaa ametusaidia’ alisema Rhyno.

Mara baada ya kugundua hilo Rhyno aliamua kutafuta namna ya kutoka kivyake, anawashukuru sana watu waliompa moyo kwani ndio waliomfanya asikate tamaa kisanii ‘kweli nilisota sana kutafuta namna ya kufanikiwa kisanaa lakini mama yangu nae hakuwa nyuma kunipa sapoti mpaka leo unaweza kuona hapa nilipofikia.

Msanii Bamboo kutoka nchini Kenya ndiye alinikutanisha na Ambroce wa Mandugu Digital, kama zali nikaweza kufanya wimbo wa ‘usipime’ ambao ndani yake kuna mistari ambayo inashabihiana kabisa na ukweli wa maisha yake yaliyomzunguka.

‘katika ngoma hii kweli kuna baadhi ya mistari ambayo nimeimba ukweli mtupu wa vitu ambavyo nimewahi kukabiliana navyo katika maisha yangu kwa mfano mstari ‘rafiki wa kweli bado mimi simjui, nashangaa hata ndugu yangu wa damu kumbe ni adui’

Kitu pekee ambacho Rhyno anapenda mashabiki wake wajue ni kwamba ‘watu wangu napenda wafahamu kuwa najituma sana mpaka nawapa kile kitu roho yao inataka wasidhani kwa kuwa kaka yangu ni supa staa ndio natoka kwa kupitia mgongo wake, hivyo kama kuna mtu anajiamini anaweza kusimama kama meneja katika kuzisimamia kazi zangu ruhsa mlango uwazi ila awe anajua wajibu wake kwa msanii’

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:14}

Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents