Burudani

Profesa J: Mez B alikuwa na ndoto nyingi, alitaka kurekebisha makosa aliyofanya kwenye muziki

Profesa Jay amesema Mez B amefariki akiwa na matumaini na ndoto nyingi na kwamba alitaka kurekebisha makosa aliyoyafanya kwenye muziki.

10957337_854475311285898_1873799816_n
Prof amepost picha hii kwenye Instagram na kuandika: Hii ni pale LEADERS CLUB kwenye msiba wa Ngwear tukitafakari na kupanga jinsi ya kwenda kumpumzisha mwenzetu, Sasa nawe umekwenda Tangulia mwanangu nasi tunafuatia, Tutakukumbuka Daima!! R.I.P MEZ B

Akiongea kwenye kipindi cha Dundo cha Mambo Jambo Radio ya Arusha, Prof alidai kuwa Mez B aligundua kuwa aliliridhika na mafanikio madogo aliyokuwa nayo na hivyo kumfanya apotee.

“Kusema ukweli alikuwa na ndoto nyingi sana za kufanya muziki na hapa mwisho alikuwa anaongea kwamba alijua makosa yake aliyofanya kwenye muziki na wasanii wengi wa muda mrefu tulikosea nyuma kwasababu tulikuwa tunaridhika na mafanikio madogo tuliyokuwa nayo,” alisema Profesa.

“Kwahiyo alikuwa anataka kutumia muda huu kujirekebisha na kufanya maendeleo ya muziki wake.”

Mez B amefariki Ijumaa hii akiwa kwao mjini Dodoma kwa kusumbuliwa na Pneumonia na uti wa mgongo. Alikuwa mtoto pekee kwa mama yake. Hajaacha watoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents