Burudani

Profesa Jay achukua kadi ya CHADEMA, kuna uwezekano akagombea ubunge 2015

Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

BKyJhNICYAAhxDi

Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu. Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.

BKyHwv0CYAAdfH5

Profesa ameamua kuweka wazi uamuzi wake baada ya watu wengi kuanza kumuuliza maswali. “Mmeniuliza sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu litapatikana Muda sio mrefu!! Still in Dodoma STAY TUNED,” alitweet.

Rapper huyo anayejulikana kama mchawi wa rhymes yupo Dodoma pamoja na wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee kwa mwaliko wa Sugu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents