Burudani

Profesa Jay: Dunia sio mahali salama kwa kuishi

Rapper Profesa Jay anazidi kuumizwa na vitu vinavyozidi kuendelea hapa nchini kwa sasa.

Jay ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mikumi, ameandika ujumbe kwenye mtandao wa Instagram ambao ndani yake unakemea vitendo viovu vinavyoendelea.

“Dunia pamekuwa sio mahali salama pa kuishi sio kwa sababu watu wabaya wana nguvu sana BALI ni kwa sababu watu WEMA wanakaa kimya na kuacha kukemea mambo mabaya – ALBERT EINSTEIN #Tupaze sauti zetu tulikomboe TAIFA @jongwe__,” ameandika katika mtandao huo.

Profesa amenukuu ujumbe huo kutoka kwa msomi wazamani wa Ujerumani ambaye anafahamika kama Albert Einstein ambaye alifariki April 1955 akiwa na umri wa miaka 76 .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents