Habari

Professa kumchapa mtu kwa Knock Out

Professor JayNajulikana kama Nigga Jay, Jay Wa Mitulinga, The Heavy Weight Mc, Daddy a.k.a Professa Jay hivi karibu ameachia jiwe lake video yake mpya inayokwenda kwa jina ‘hapo sawa’ ikiwa imetengenezwa na…

Pressor Jay


Najulikana kama Nigga Jay, Jay Wa Mitulinga, The Heavy Weight Mc, Daddy a.k.a Professa Jay hivi karibu ameachia jiwe lake video yake mpya inayokwenda kwa jina ‘hapo sawa’ ikiwa imetengenezwa na kampuni nambari wani katika utengenezaji wa Mavideo ya ukweli kabisa na makali ya Visual Lab.


“huu ni mwanzo wa maandalizi ya albam yangu ‘Aluta Continua’ ambayo natarajia itakuwa ni moja kati ya albam zitaingia katika masoko ya muziki kimataifa, ambapo mpaka sasa ni singo moja ambayo imeshasikika ambayo ni ‘ndivyo sivyo’ nikiwa na Chameleone then nyingine ambayo imeonekana luningani ambayo ni ‘hapo sawa’ iliyorekodiwa katika studio za 41 Record na prodyuza Ambrose”


katika video hiyo Professa Jay anaonekana akiwa ulingoni kama mwanamasumbwi ambapo anampa kichapo cha Knock out mpinzani wake na kuibika mshindi, pamoja na hayo pia kuna wasanii wenzani kibao ambao wameuza sura katika video akiwemo mangwea, Fid Q, Geez na wengine kibao.


Albam itakwenda kwa jina la ‘Aluta Continua’ ambapo ameiunda katika mlengo wa kimataifa kwa kushirikiana na wasanii kibao wa ndani na nje ya nchi….stay tuned.


Sikiliza “Hapo Sawa”
{play}prof_jay_hapo_sawa.mp3{/play}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents