Professor Jay aamua Kung’atuka

Professor Jay ameamua kung’atuka kwenye game na kuamua kumrudia Mungu huku akiendelea kujutia mambo yote ambayo ameikosea jamii, ikiwa ni maneno yake yaliyofungamana na maudhui yanayosikika katika singo yake mpya

Professor Jay


Msanii wa kizazi Kipya Joseph Haule a.k.a Professor Jay ameamua kung’atuka kwenye game na kuamua kumrudia Mungu huku akiendelea kujutia mambo yote ambayo ameikosea jamii, ikiwa ni maneno yake yaliyofungamana na maudhui yanayosikika katika singo yake mpya ambayo ameiachia hivi karibuni katika vituo mbali mbali vya redio inayokwenda kwa jina la ‘nang’atuka’.


 


Katika singo hiyo Prof amegusia mambo mengi ambayo kiongozi yoyote anaweza kuyafanya wakati akiiongoza jamii ya aina Fulani, hasa anapokuwa na malengo ya kuchuma kupitia migongo ya raia ambao anawaongoza.



“Nang’atuka nimeshaikosea jamii nikajiita Mungu mtu, Nikajiita Nabii, Nang’atuka Mwenyezi kumbuka na nafsi hii, napiga goti natubu daima nitakutii” hayo ni maneno yake ambayo yanasikika katika kiitikio cha songi hilo ambayo limesheheni mistari yenye hisia kali na inayoilenga jamii moja kwa moja.


 


Haya ni maandalizi ya ujio wa albam mpya ya msanii huyu itakayojulikana kwa jina la ‘Aluta Kontinyua’ ambapo mpaka kufikia tarehe 4 Mwezi anatarajia kupiga bonge la Show ndani ya ukumbi wa Dimond Jubele nah ii ni baada ya kukaa zaidi ya miaka mitatu bila ya kufanya uzinduzi jijini Bongo.



“Natarajia kufungua maktaba zangu nikiwa na maana nahitaji kupiga show tangu nilipoanza kufanya michano na kundi langu la Hard Blasters ambapo wanajeshi wangu wote watatimba jukwaani na kufanya makamuzi ya kufa mtu, kwa kweli sio k=siku ya kukosa kwani najua mmenimiss kama ambavyo na mimi nimewamiss kuwaona mkinishangilia niwapo Jukwaani” alisema Prof alipokuwa akipiga stori na mshika kalamu wa Bongo5.com


 


Bofya hapa kusikiliza Nang’atuka ya Professor Jay

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents