Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Professor Jay ampigia saluti Diamond Platnumz ‘umekuwa mfano bora’

Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kukiri wazi kuwa mtoto wa Mwanamitindo, Hamisa Mobeto kuwa ni wa kwake. Hatimae Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule a.k.a Professor Jay amempongeza mkali huyo kwa kitendo hicho.

Diamond Platnumz na Professor Jay

Professor Jay amesema Diamond Platnumz kwa kitendo hicho amekuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii kwani kuna watu wengi wanapitia changamoto kama hizo.

Ukweli humuweka Mtu huru kweli kweli, Big up mdogo wangu @diamondplatnumz Umekuwa Mfano bora sana,“ameandika Professor Jay kwenye ukurasa wake wa Twitter.

SOMA ZAIDI – Diamond Platnumz akiri mtoto wa Hamisa Mobeto ni wa kwake

Mwezi Juni mwaka huu kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond Platnumza alikana ujauzito wa Hamisa Mobeto huku akimtaka amtaje baba halali wa mimba hiyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW