Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Professor Jay awachana wasanii ambao hawamsupport kwenye muziki ‘nisiwaone tena’

Msanii wa muziki wa hip hop, Professor Jay ambaye ni mbunge wa Mikumi, amefunguka kwa kudai kwamba kuna baadhi ya wasanii wanashindwa kumsupport licha ya yeye kuwaonyesha support kwenye muziki wao.

Rapa huyo ambaye kwa anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Yatapita’amesema yeye anakuwa mwepesi kwenye kuwasupport wasanii wenzake lakini anashangaa kwanini wao wanashindwa kumsupport.

“ATTENTION PLEASE🔥🔥🔥.Hii ni kwa wasanii wenzangu wote ambao kila nikitoa KAZI zangu wanauchuna kama hawanioni na hawataki Kunisupport ila wao kila siku wapo kwenye inbox yangu wakiomba niwapost na ninafanya hivyo mara kwa mara,
Kuanzia sasa Hivi msije tena INBOX kwangu maana mtakutana na HII😏
#yatapita Video ipo kwenye BIO👆🏻,” aliandika Professor Jay.

Bongo5 ilimtafuta rapa huyo na kusema kwamba ni kweli kuna baadhi ya wasanii wanashindwa kumsupport wakati yeye huwa anawasupport.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW