Burudani

Professor Jay na Ben Pol wamvuta Harmonize, mwenyewe asema ametimiza ndoto yake kukutana nao

Good News kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva hususani wale wanaopenda kazi za Ben Pol, Harmonize na Professor Jay kwani tayari kolabo kati ya watatu hao inanukia.

Kolabo hizo zimethibitishwa jana na Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kolabo na Ben Pol na Professor Jay zote zitakuwa ngoma za kushirikiana.

Harmonize amesema leo wanaanza ku-shoot video na Ben Pol na huku posti yake ya pili akionesha video akiwa studio  na Professor Jay huku akieleza kuwa tukio hilo kwake ni kutimiza ndoto ya muda mrefu ya kutamani kufanya kazi na mkongwe huyo wa Hip Hop.

Harmonize kwa mwaka huu amefanya kolabo kibao na zote zimekuwa hit ikiwemo Kwangwaru na Diamond Platnumz, nimwage radhi na Mrisho Mpoto, DM Chick na Sarkodie na nyingine nyingi.

Related Articles

4 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents