Burudani

Professor Jay ni mbunge mteule wa Mikumi

Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Professor Jay amechaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro.

Professor akiwa kwenye shughuli za kisiasa

Jay ambaye alikuwa anawania ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA, ametangazwa rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 32,259 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Jonas Nkya wa CCM aliyepata kura 30,425.

Kwa mujibu wa ITV, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Mikumi amemtangaza rasmi Professor Jay kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.

Professor hakuchelewa kusambaza habari hiyo njema kwa mashabiki wake kwa kuandika kwenye Instagram: Jimbo la Mikumi Joseph Haule (CHADEMA) Kura 32259, Jonas NKYA (CCM) Kura 30425, Tumeshinda kwa tofauti ya kura 1834. Asante Mungu.”

Rapper huyo anakuwa mbunge wa pili kuingia bungeni baada ya Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi aliyeshinda pia ubunge wa Mbeya Mjini kwa mara ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents