Promota maarufu, David Higgins amuonya Anthony Joshua kutomdharau Parker

Promota maarufu nchini New Zealander, David Higgins amemuonya bingwa wa dunia wa uzito wa juu nchini Uingereza, Anthony Joshua kutomdharau hata kidogo mpinzani wake, Joseph Parker na kumzungumzia Deontay Wilder bali kuweka mawazo yake yote kwa mwanamasumbwi huyo atakaye kutana naye ulingoni mwishoni mwa mwezi huu uwanja wa Cardiff.

Higgins ameyasema hayo katika kipindi hiki ambacho bingwa huyo  wa dunia wa uzito wa juu wa WBA na IBF, Anthony Joshua akielekea katika pambano lake la kihistoria dhidi ya Joseph Parker litakalo pigwa Machi 31 mwaka huu.

Anthony Joshua atakuwa anakosea kama ataacha kumfikiria mpinzani wake Parker nakuwaza mambo mengine ambayo yapo nje ya pambano lake lijalo, Higgins amekiambia chombo cha Sky Sports.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW