Michezo

Promota wa Joshua atoa onyo kali kwa timu nzima ya Joseph Parker

Promota wa Anthony Joshua, Eddie Hearn ameitaka timu ya Joseph Parker kuzungumza maneno yao ya kishujaa mbele ya mpinzani wao na sio kuyasemea pembeni.

Hearn ameyasema hayo mbele ya promota wa Parker, David Higgins.

Bondia huyo anaeshikilia mkanda wa WBO atakuwa na kibarua kizito dhidi ya Joshua kuwania mkanda wa WBA na IBF ubingwa wa uzito wa juu mchezo utakao pigwa Machi 31 siku ya Jumamosi.

Nahitaji wao wazungumze mbele ya Anthony  Joshua kwasababu ‘AJ’ alihitaji waseme mbele yake.

Nilimwambia baadhi ya maneno waliyozungumza watu wake kwa kuwa angependa kuskia.

Lakini kama nilivyosema kwa Higgins na hili liende kwa timu yake nzima ya Parker wasijifungie vyumbani na kuhitisha kijimkutano kido na waandishi wa habari huko New Zealand waje wakutane na sisi Jumanne waseme mambo yote hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents