Michezo

PSG kuanza kuonyesha nguvu ya pesa leo Uefa

Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya inatarajia kuanza kutimua vumbi hii leo katika viunga mbalimbali huku kubwa ikiwa ni ujio wa kishindo wa matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain ambayo inatizamwa kuleta ushindani mkubwa katika michuano hiyo ya mwaka huu.

                                                       Neymar da Silva Santos Júnior  

Paris St-Germain, ikiwa chini ya rais wake, Nasser al-Khelaifi inaonekana kuwa tishio baada ya kufanya usajili mkubwa uliyoweka rekodi ya dunia kwa kumsajili mchezaji raia wa Brazili na klabu ya Barcelona, Neymar da Silva Santos Júnior  kwa dau la paundi milioni 222 huku ikifanikiwa kumchukua kinda wa AS Monaco, Kylian Mbappe  hivyo kuwa na muunganiko bora kabisa msimu huu.

PSG inayopata kiburi kutoka kwa wafadhili wake mashekh wa Qatar wataingia uwanjani leo wakiwa ugenini katika mchezo wa kundi B kupepetana na timu ya Celtic katika dimba la Celtic Park – Glasgow.

                                                                         Kylian Mbappe

Mabingwa marambili mfululizo wa klabu bingwa barani Ulaya timu ya Real Madrid wanatarajia kuingia dimbani hapo kesho kukipiga dhidi ya klabu ya Apoel Nicosia.

Baada ya kuwa klabu ya kwanza kushinda kombe kwa miaka miwili mfululizo , katika ligi ya klabu bingwa ulaya, Real Madrid tayari imeweka historia.

Lakini swali ni iwapo wataweza kulitetea taji hilo kwa miaka mingi kufuatia matokeo ambayo yamekuwa wakishuhudia kutoka kwa wachezaji ambao waliwatangulia misimu mitano iliyopita na kushinda kombe la ulaya tangu kuazishwa kwa ligi hiyo mwaka 1956.

Kuna dalili nzuri za kupata ushindi.Ni mara chache ambapo timu hufuzu katika ligi ya vilabu bingwa ikiwa na kikosi kikali.

Si kwa kawaida kwamba Real katika kipindi cha pili wakati walipokuwa wakikabiliana na Juventus mwezi Juni katika fainali huko Cardiff iliwavutia wengi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu katika uwanja wa Bernabeu.

Klabu hiyo ilidhihirisha kwamba kuna mipango katika siku za mbeleni ya kuwatengemea wachezaji nyota.

Klabu hiyo imekuwa ikiwateuwa vijana wadogo wenye talanta kama Marco , Asensio, Dani Ceballos na wachezaji wengine wa klabu hiyo mbali na kocha wao Zinedine Zidane ambaye amekuwa akiwateuwa wachezaji hao kutokana na ujuzi na sio kulingana na nafasi yao katika jamii.

Iwapo Real Madrid wamerudi nyuma kwa kuwasajili wachezaji wakati wa uhamisho , hapo basi PSG wamejinyakulia nafasi kwa namna nyengine.

Usajili wa Neymar uliwashangaza wengi katika ulimwengu wa soka, na ilionekana kama mwanzo mpya kwa Wafaransa hao.

Kufuatia matokeo ya klabu hiyo tangu uwekezaji wa kutoka Qatar (QSI) mwaka 2011, klabu hiyo ilikuwa haijawahi kuwa na uwezo wa kufanya usajili wowote kwa wachezaji wa hali ya juu hadi hivi sasa.

Huku akishirikiana na kinda wa Ufaransa Kylian Mbappe aliyeiaga Monaco na kuelekea Parc des Princes, Neymar bado ataendelea kuwa miongoni mwa wachezaji watatu wa Ulaya lakini kwa hivi sasa mambo yatakuwa na uso mpya.Timu hiyo sasa inawashambuliaji nyota watatu Neymar, Mbappe na Edinson Cavani.

Bidii ya Barcelona kuishinda PSG walipokuwa wakikabiliana dhidi ya PSG waliotoka sare katika hatua ya timu kumi na sita bora ilisababishwa na bidii na jitihada za Neymar.

Bado klabu hiyo imeachwa mdomo wazi baada ya raia huyo wa Brazil kuhamia Ufaransa huku shida ambazo mabingwa hao wamekuwa wakikumbana nazo uwanjani na katika vyumba vya mikutano sasa zimewekwa hadharini.

Neymar angekatazwa kuihama klabu hiyo lakini haikuwezekana kwani alikuwa amekosa matumaini na usimamizi wa Barcelona.

Lionel Messi bado hajasaini muda zaidi wa mkataba wake ambao utakamilika msimu huu, baada ya rais ambaye anakumbana na changamoto , Joseph Bartomeu kudai kwamba kiungo wa kati Andres Iniesta alitarajiwa kutia saini mkataba mpya mbele ya umma na akakataa.

Ni msimu wa historia kwa timu za Uingereza , zikiwemo timu tano katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza , Manchester United walifuzu kupitia ligi ya Uropa na wataungana na mabingwa wa Scotland Celtic baada ya kuonyesha matamanio yao ya kujiunga na michuano hiyo.

Kikosi cha Jose Mourihno kimeonekana kurudi katika michuano hiyo na kuwa kileleni katika kundi lao, licha ya kwamba Benfica ni wapizani ambao hawastahili kudharauliwa.

Chelsea wanakumbana na Atletico Madrid huku Manchester City wakistahili kuwa macho kwa mashambulizi ya Napoli na timu ya Ukraine ya Shakhtar Donetsk, ambayo imevunja rekodi chini ya meneja Paulo Fonseca msimu uliopita.

RB Leipzig inatarajia ushindani mkali , wamewekwa katika kundi lililoko katika kiwango sawa pamoja na mabingwa wa Ufaransa Monaco, Besiktas na Porto.

Hata upande wa Ralph Hasenhuttl wamefanya kazi ngumu zaidi kwa kumtumia Naby Keita na Emil Forsberg katika safu yake ya kati.

Timo Werner atafunga mabao na winga aliyesainiwa upya Bruma ni kiungo machachari. Leipzip kwa hivi sasa wanafahamu jinsi ya kujiimarisha.

Napoli ni farasi mweusi katika hatua za hapo mbeleni.

Katika timu za ligi ya Serie A, AC Milan imeonyesha mabadiliko katika kipindi cha dirisha la uhamisho , upande wa Maurizio Sarri wameamua kuwa dhabiti na wameamua kuwatumia Dries Mertens, Jose Callejon na Lorenzo Insigne.

Huku katika kiungo cha kati wakiwa na matarajio ya kumtumia Marek Hamsik ambaye yuko karibu kufikia rekodi ya ufungaji magoli ya Diego Maradona ambayo wanajaribu kuipiku.

Ratiba ya Klabu bingwa barani Ulaya wiki hii

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents