Pure Academy kumsomesha Miss Tanzania
Chuo cha Pure Academy of Aesthetics kimetoa schorlaship kwa Britney Urassah mrembo kutoka katika kambi ya Vodacom Miss Tanzania 2010 kujifunza urembo kwa undani zaidi.
Kigezo kikubwa walichoangalia ni mrembo ambaye alikuwa na uelewa wa hali ya juu, mcheshi na anayependelea mambo ya urembo na mwenye kuongea vizuri.
Director wa Chuo hicho Hanif Virani alisema chuo cha Pure Academy Aesthetics kinatoa kozi tatu ambazo ni Hair,Beauty pamoja na Make up na kikiwa na malengo ya kuwaelimisha vijana kupata elimu ya urembo kimataifa,”Tanzania imefunguka na ni nchi ya kimataifa na tunaweza kufanya na ndio maana tumeanza”
Alisema kuwa chuo hikcho kimempa schorlaship Britney kusoma kozi zote tatu na kwa jinsi atakavyoonyesha biidii anaweza kupata ajira papo hapo.Hanifu alisema ,’Nadhani elimu tutakayoitoa itasadia katika jamii yetu, kutambua kuwa urembo siyo kubadilisha rangi ya ngozi kwani hii ni changamoto kubwa ambayo ipo mbele yetu na mambo mengi tu yanayohusu urembo kwani nimegusia hilo moja ikiwa ndio changamoto kubwa.’
Chuo hiki kimenza hivi karibuni na tunategemea kuleta mabadiliko makubwa katika mambo ya hair beauty na make up hapa nchini Tanzania,kwa sasa nina wanafunzi 12 ambao wao ndio intake ya kwanza.