Michezo

”Pyramids FC inafungika ni timu ya kawaida tu, sisi ndiyo wenye nchi wale wengine ni wahamiaji” Kaimu Katibu Mkuu Yanga

Kaimu Katibu Mkuu wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC, Dismas Ten amesema kuwa timu yake inayo uwezo wa kuwafunga wapinzani wao klabu ya Pyramids FC katika mchezo wa kombe la shirikisho unaotarajiwa kupigwa wiki chache zijazo.

Ten ameyasema hayo kupitia akaunti yake ya Instagram, huku akijinasbu kuwa Pyramids FC ni timu ambayo inafungika na wanakilasababu ya kupata ushini kwenye mchezo huo.

”Nimewatizamaa hao jamaa naona ni timu ya kawaida ambayo inafungika pia, kitu muhimu kwetu ni maandalizi ya kutosha, kila mmoja awajibike kwenye eneo lake, tuna kila sababu ya kushinda mchezo wa kwanza tarehe 27/10 kisha tukamalizie shughuli huko kwao. Wananchi /wenyenchi ndiyo sisi wale wengine wahamiaji tu wasitutingishe..! Kabiiiisa.” Ameandika Dismas Ten.

Kumekuwa na maneno maneo kwenye mitandao ya kijamii hasa kutoka kwa mashabiki wa soka nchini wakidai kuwa Pyramids FC ni timu yenye kiwango bora na yenye kikosi cha gharama kubwa ukilinganisha na wapinzani wao Yanga.

https://www.instagram.com/p/B3erSg4g5g6/

Pyramids FC msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu ( 3) nyuma ya Zamalekh na mabingwa Al Ahly wakiwa hivyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu huu (2019/20).

Matokeo ya michezo yake ya kwanza kwenye michuano hiyo ya Shirikisho Pyramids matokeo yalikuwa kama ifuatavyo. Pyramids 4-1 Etoile du Congo, Etoile du Congo 0-1 Pyramids.

Kisha klabu hiyo ya Misri, ikakutana na Belouizdad ya Algeria na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo kwa mchezo wa nyumbani na ugenini. Pyramids 1-1 Belouizdad, Belouizdad 0-1 Pyramids.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents